Jiunge nasi

Kuhusu Kiswahili.co.ke

Mtandao huu umejitolea kwa sababu ya kutumia teknolojia ili kukuza somo la Lugha ya Kiswahili.

Malengo makuu

Mtandao huu unajitahidi kufikia malengo ya kipekee katika jamii;

  • Kukuza lugha ya kiswahili kupitia mtandao - Kwa sababu mambo mengi ya kijamii hufanyika kwenye mtandao, mtandao huu umejitolea kukuza lugha ya Kiswahili kwa kuelimisha jamii mtandaoni
  • Kutumia teknolojia kufunza na kukuza Kiswahili - Tovuti hii ni moja baadhi ya mbinu za kukuza na kufunza Lugha ya Kiswahili. Hili lengo linaafikiwa kwa sababu, tovuti hii imejengwa kutumia Lugha ya Kiswahili pekee yake na shughuli zake zote zinaendeshwa kwa Lugha sanifu ya Kiswahili.
  • Kituo cha wanafunzi, walimu na hata vyuo vya Kiswahili - Lengo hili la kipekee litaafikiwa kwa kutumia teknolojia kueleza wahusika mbali mbali umuhimu wa kijiunga na kutumia mtandao wa Kiswahili.co.ke , ili pamoja Kiswahili kikuzwe.

Wanafunzi

Walimu

Mitihani

Kongamano

Nguzo Kuu

Kila jambo linahitaji nguzo za kulilinda. Nguzo hizo husaidia kuhakikisha malengo fulani yametimia. Hizi baadhi ya nguzo za mtandao huu.

Ubunifu

Kiungo cha ubunifu ni nguzo muhimu katika mtando huu, mtandao huu unatumia teknolojia kwa njia bunifu ili kukuza Lugha ya Kiswahili.

Uaminifu

Mtandao huu unaweka taarifa, masomo, na jumbe za kuaminika baada ya kufanya utafiti kutoka kwa waliohitimu kwenye nyanja mbalimbali za Kiswahili.

Ushirikiano

Kidole kimoja hakifunji chawa. Mtandao huu unawashirikisha wanataaluma mbali mbali, kwa mfano; wanaotengeneza tovuti, walimu, wanafunzi na hata vyuo vya Kiswahili ili kwa pamoja kufanikisha malengo ya Kiswahili.co.ke